November 14, 2024

Information reaching Kossyderrickent has it that Damas Clinton Nyundo anatajwa kuwa ni askari watano wa JWTZ soldiers waliombaka afisa wa kike wa polisi katika kanda ya ngono iliyovuja kwa virusi nchini Tanzania.

 


 



Wakati jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wa tulio la udhalilishaji wa binti linaloonekana kwenye video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya jana, limewataka wenye video hizo kuzifuta mara moja na kuacha kuzisambaza.

Polisi imesema hayo kupitia taarifa aliyoitoa, Msemaji wake, David Misime, leo Agosti 4, 2024 kwamba watu wanaofanya hivyo ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015.

“Jeshi la Polisi tulitoa taarifa ya kusambazwa katika mitandao ya kijamii, picha ambazo zinamwonyesha binti mmoja akifanyiwa vitendo vya kikatili ambavyo ni kinyume na sheria, utamaduni wa Mtanzania na kinyume cha haki za binadamu.

“Tulieleza, Jeshi la Polisi tulishaanza kulifanyia kazi tukio hilo ambalo ni la kinyama na la kulaaniwa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

 Aidha, “tulitoa wito watu wasiendelee kusambaza picha hizo kwani ni kinyume na sheria lakini pia kwa kufanya hivyo ni kuendelea kumfedhehesha na kumtesa kisaikolojia Mtanzania mwenzetu huyu.”

Polisi imesema pamoja na wito huo bado wapo baadhi wanaendelea kusambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii na kutumiana kwenye makundi mbalimbali.

“Kutokana na vitendo hivyo, Jeshi la Polisi linaelekeza wanaofanya hivyo waache mara moja Pia, kwa yeyote yule mwenye picha hizo azifute,” imeeleza taarifa hiyo.

Mapema hii leo, zilisambaa video za tukio la kikatili lililodaiwa kufanywa na wanaume watano dhidi ya msichana (jina halijafahamika), anayedaiwa kuwa mkazi wa Yombo Dovya, Wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam.

Msichana huyo anadaiwa kubakwa na kuingiliwa kinyume na maumbile na vijana hao wanaodai kupitia video hiyo kuwa, wametumwa na afande wakimtuhumu (msichana) kutembea na mume wa mtu.

Kipande cha video kinachosambaa mitandaoni kinaonyesha jinsi vijana hao walivyotekeleza tukio hilo ambalo tayari Polisi na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalumu, Dk Dorothy Gwajima wamelilaani.


Discover more from KossyDerrickent

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Discover more from KossyDerrickent

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading